Serikali Yakubali Mchango wa Shule Binafs
Serikali Yakubali Mchango wa Shule Binafs
ELIMU

SERIKALI imesema inatambua na kuunga mkono mchango wa elimu unaotolewa na wamiliki wa shule binafsi katika maeneo mbalimbali hapa nchini na imeahidi kuwa nao bega kwa bega ili kuendelea kuboresha elimu.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Chama cha Wawekezaji Binafsi katika Elimu Tanzania (TAPIE) unaofanyika kwa siku mbili mjini hapa.
Profesa Ndalichako alisema wawekezaji binafsi kwenye sekta ya elimu kama wanaona wana changamoto wakae meza moja na wadau wenzao (serikali) ili kuzitatua.
“Kama kuna tatizo linajitokeza katika elimu tunatakiwa kuwa wamoja bila kuangalia itikadi zetu za kidini au kisiasa ili tuweza kuwasaidia watoto wetu katika elimu,” alisema.
Aidha, alisema serikali inaandaa chombo maalumu cha taaluma ya walimu ili kuhakikisha kinasimamia maslahi na viwango vya mishahara ya walimu wote nchini bila kujali ametoka serikalini au kwenye shule binafsi.
Rais wa TAPIE, Ester Mahawe aliishukuru serikali kwa kutambua umuhimu wa ushirikiano baina ya sekta ya umma na binafsi katika kuendeleza elimu nchini kuanzia elimu ya msingi hadi elimu ya juu.
“Sisi TAPIE tunakupongeza kwa kuteuliwa kuwa waziri, kwetu sisi uteuzi wako umekuja wakati muafaka maana tumeshuhudia dhamira yako ya kupenda kuona elimu yetu inazidi kuwa ya viwango bora….tunaamini chini ya ulezi wako changamoto nyingi zilizokuwa zinatukabili zitapata majawabu,” alisema.
Alisema Sera ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya Mwaka 1995 na Sera mpya ya Mwaka 2014 zinaeleza bayana umuhimu wa dhana ya serikali na sekta binafsi katika elimu hivyo wadau wa sekta binafsi wanawajibika kuchangia jitihada za serikali kuinua ubora wa elimu.
Kwa Wenye WhatsApp tu..SAVE namba 0658222008 kwenye Simu Yako, Halafu Tuma Neno" habari" Kwa WhatsApp Utapata Habari Mpya "BURE" Kila siku
Comments
Post a Comment