Posts

Showing posts from September, 2016

Wasanii na viongozi wa WCB waalikwa nyumbani kwa rais mtaafu Jakaya Kikwete

Image
Wasanii na viongozi wa WCB waalikwa nyumbani kwa rais mtaafu Jakaya Kikwete Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete Jumatano hii aliwaalika wasanii wa label ya WCB pamoja na viongozi nyumbani kwake na kula nao chakula cha mchana. JK ambaye ni mmoja kati ya marais ambaye amesupport sana wasanii wa muziki nchini, aliwaalika wasanii hao nyumbani kwake na kuzungumza nao mambo mbalimbali kuhusu muziki wao. Mmoja kati ya viongozi wa juu wa label hiyo, Sallam alimshukuru rais huyo kwa kuwaalika nyumbani kwake na kuzungumza nao mawili matatu kuhusu muziki. “Former President JM Kikwete and Former First Lady Mama Salma Kikwete. Asanteni kwa mwaliko wenu!! Allah awape afya njema,” Sallam aliandika instagram.

kutokana na habari kwamba diamond alitelekezwa.Diamond Ashauriwa kumsamehe Baba'ke

Image
Diamond Ashauriwa kumsamehe Baba'ke Ni kweli inauma mno kutelekezwa na mzazi. Mimi ambaye baba na mama yangu walinilea kwa umoja wao pamoja na umaskini wetu, huwa nawaza ingekuwaje baba au mama asingekuwa karibu yangu? Malezi ya mzazi mmoja au wote wasingekuwepo. Inaumiza sana!   Hiyo ndiyo sababu naweza kuhisi kile ambacho kinamuumiza mtoto aliyetelekezwa. Mimi ni baba, najua ni kiasi gani mtoto wangu ananihitaji kwa ukaribu. Upendo wangu kwake umekuwa zawadi yake muhimu kutoka kwangu kuliko kitu chochote. Hivyo basi, najua atapitia machungu kiasi gani kama nikimtelekeza.   Chukua hii; Kwa hali yoyote ile, mzazi hana leseni ya kumtelekeza mtoto wake. Changamoto zije na ziondoke, hakikisha unabaki umemganda mwanao. Kosa la kumtelekeza mtoto linafanana na la kuua. Huyo ni mtoto wako, unamkimbia, unataka alelewe na nani?   Mwanamuziki Aboubakar Shaban Katwila ‘Q Chilla’ katika nyimbo zake Aseme na Si Ulinizaa, alionesha wazi kuumizwa na alivyokataliwa na baba yak...

Wema Sepetu Ajipanga kumfikisha Diamond Mahakamani,ingia kwenye blog hii kupata zaidi kilichojili

Image
Wema Sepetu Ajipanga kumfikisha Diamond Mahakamani Msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu anaandaa utaratibu wa kumfikisha mahakamani aliyekuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kufuatia kitendo cha msanii wa Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Raymond ‘Rayvanny’ kumtumia kwenye video ya wimbo wake wa Natafuta Kiki bila makubaliano.  Akizungumza nasi hivi karibuni, Wema alisema amefikia uamuzi huo kutokana na Diamond kukiuka makubaliano waliyofanya awali kuhusu yeye kuonekana kwenye video hiyo. Alisema: “Diamond alinifuata na kunitaka nionekane kwenye video ya msanii wake Raymond, nikamwambia anipe milioni 10, yeye akaonesha alikuwa anataka free huku akisema mbona nilimsaidia Ommy Dimpoz. “Nilimwambia kuwa nilimsaidia Dimpoz kwa kuwa alikuwa anahitaji msaada lakini yeye nilitaka anipe kiasi hicho cha pesa. “Baadaye niliongea na Martin Kadinda kuhusu kile alichotaka Diamond na pesa ambayo nilimtajia, Martin akaniambia kwa ishu hiyo hata milioni 10 ni ndogo, nikashituka...

Video Mpya : P-Square – Bank Alert,ingia kwenye blog hii kuwatch na kudownload

Image
Video Mpya : P-Square – Bank Alert Baada ya kuvunjika kwa kundi la P-Square linaloundwa na ndugu wawili, Peter na Paul Okoye huku kila mtu akifanya kazi kivyake, hatimaye kundi hilo limerudi tena kwa wasanii hao kuachia video ya wimbo wao mpya ‘Bank Alert.  Tazama hapa chini video hiyo. ==

Serikali Yakubali Mchango wa Shule Binafs

Image
Serikali Yakubali Mchango wa Shule Binafs     ELIMU     SERIKALI imesema inatambua na kuunga mkono mchango wa elimu unaotolewa na wamiliki wa shule binafsi katika maeneo mbalimbali hapa nchini na imeahidi kuwa nao bega kwa bega ili kuendelea kuboresha elimu. Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Chama cha Wawekezaji Binafsi katika Elimu Tanzania (TAPIE) unaofanyika kwa siku mbili mjini hapa. Profesa Ndalichako alisema wawekezaji binafsi kwenye sekta ya elimu kama wanaona wana changamoto wakae meza moja na wadau wenzao (serikali) ili kuzitatua. “Kama kuna tatizo linajitokeza katika elimu tunatakiwa kuwa wamoja bila kuangalia itikadi zetu za kidini au kisiasa ili tuweza kuwasaidia watoto wetu katika elimu,” alisema. Aidha, alisema serikali inaandaa chombo maalumu cha taaluma ya walimu ili kuhakikisha kinasimamia ma...

MPYA:TAMISEMI YATOA UFAFANUZI KUHUSU UHAMISHO NA AJIRA ZA UALIMU 2015/2016

Image
J MPYA:TAMISEMI YATOA UFAFANUZI KUHUSU UHAMISHO NA AJIRA ZA UALIMU 2015/2016  AUTHOR BY DAVID MABINA Hivi karibuni kumezuka tabia za utapeli unaofanywa na wanaojisadikisha kuwa ni watumishi wa Umma au Mawakala wa kusimamia uhamisho wa Watumishi kuhama kutoka Mkoa mmoja kwenda Mkoa mwingine na pia kujihusisha  na kutoa taarifa za uongo kwa   kugushi nembo za Ofisi ya Rais. – TAMISEMI kuhusu ajira, kupandisha madaraja ya walimu. Yamekuwepo Malalamiko mengi kutoka kwa wahanga/waathirika wa tabia hiyo kwa nyakati tofauti ambayo watumishi wamehadaiwa kuwa watasaidiwa kuhamia sehemu yoyote wanayoihitaji baada ya kulipa kiwango cha fedha ambacho hupangwa na wahalifu hao. Miongoni mwa taarifa batili wanazosambaza ni Uhamisho na Ajira za Walimu. Matangazo hayo pia yameonekana katika mbao za matangazo za baadhi ya Halmashauri. Mara nyingi watu hao huweka namba zao za simu kwa ajili ya kupokea fedha za uhamisho kutoka kwa watumishi pamoja na kuweka anuani za barua pe...
Image
Thursday, September 15, 2016 author:david mabina Watano kortini kwa kumdhalilisha Rais Magufuli VIJANA watano wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumdhalilisha Rais Dk. John Magufuli na Jeshi la Polisi kutokana na mauaji ya askari polisi wanne waliouawa na majambazi katika eneo la Mbande na Vikindu, Dar es Salaam hivi karibuni. Washtakiwa hao walifikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya mahakimu watano tofauti na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Salum Mohammed. Walisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Emmilius Mchauru, Huruma Shahidi, Margareth Bankika, Dk. Yohana Yongolo na Respicius Mwijage. Akisomewa mashtaka, mshtakiwa Dennis Mtegwa anadaiwa Agosti 24, mwaka huu eneo la Ubungo External kupitia mtandao wa WhatsApp, aliweka maoni katika group linaloitwa Dsm 11 4u Movement, akisema ‘JPM sijui anawaza nini kichwani… hata samahani hajui au nilikosea hajui’, ‘nchi imefika hapa kwa sababu ya mtu mmoja...

WALIOCHAGULIWA NA CHUO KIKUU CHA MARIAN MWAKA 2016/2017

Image
<<CLICK HERE TO SEE NAMES BACHELOR FIRST ROUND STUDENTS SELECTED 2016/2017---PDF>>    
Image
                                                                                                                       MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA VYUO VIKUU MBALIMBALI 2016/2017  Mabina david    Kama kawaida yetu  MABINADAVID.COM  katika nusanusa yetu tumefanikiwa kunasa hii ambayo ilikuwa ikisubiriwa na watu wengi,ni kuhusu majina ya wanafunzi waliochaguliwa na TCU 2016/2017 kujiunga vyuo vikuu mbalimbali 2016/2017.   wale wote mlioomba vyuo kama, Chuo Kikuu cha Ardhi, (ARU) Chuo Kikuu cha Hubert Kairuki (HKMU), International Medical and Technological University (IMTU) Moshi University College of Cooperative and Business ...